1. Update ya Usalama ya Februari 2026 (Security Patch)
Samsung wameanza kutoa update ya usalama ambayo inarekebisha vudhaifu (vulnerabilities) 37 kwenye mifumo yao.
Zinazorekebishwa: Matatizo kwenye mfumo wa biometrics (fingerprint na face unlock), usalama wa app ya Settings, na Samsung Dialer.
Simu zinazoanza kupata: Ni mfululizo wa Galaxy S26, S25, S24, na simu mpya za kukunja kama Z Fold 7 na Z Flip 7.
2. Mabadiliko ya Support (S21 na S22)
Kuna habari za kusikitisha kwa watumiaji wa simu za zamani:
Galaxy S21, S21+, na S21 Ultra: Rasmi zimeondolewa kwenye orodha ya kupata update za kila mwezi. Update ya Januari 2026 ndiyo ilikuwa ya mwisho ya kila mwezi; kuanzia sasa hazitapata updates mara kwa mara.
Galaxy S22 Series na S21 FE: Zimeshushwa daraja (demoted). Sasa zitakuwa zinapata update mara moja kila baada ya miezi mitatu (Quarterly) badala ya kila mwezi.
3. Maandalizi ya One UI 8.5
Samsung wameanza kufanya majaribio ya One UI 8.5 (inayotokana na Android 16) kwa baadhi ya simu za katikati (mid-range) kama Galaxy M33 5G na Galaxy M06. Update hii inatarajiwa kuleta maboresho zaidi kwenye mifumo ya Galaxy AI na muonekano mpya wa animations

Comments
Post a Comment